Waziri wa Afya, Ustawi
wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui ameahidi kudumisha
ushirikiano uliopo kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri
ya watu wa China ili kuinua Uchumi wa Nchi.
Akizungumza na Balozi
Mdogo wa China aliopo Zanzibar na ujumbe wake, wakati akipokea msaada wa
Dawa kutoka Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China Mhe. Mazroui amesema Serikali
hizi mbili ni marafiki wa muda mrefu hivyo wataendeleza ushrikiano huo ili
kuwapatia wananchi huduma bora za afya.
Aidha amesema Serikali
ya Zanzibar inaishukuru Serikali ya Jamuhuri ya watu wa China kwa kushirikiana
nao kwa kila hali pamoja na kuwapatia misaada mbali mbali ikiwemo Dawa,
Madaktari na Chanjo ya UVIKO-19.
“Tunishukuru Serikali
ya Jamuhuri ya watu wa China wamekuwa wakishirikiana na sisi kwa kila hali
hususani Wizara ya Afya kwa kutupatia madaktari kila mwaka na misaada mbali
mbali ambayo husaidia katika kutoa huduma kwa wananchi” alisema Waziri.
Mapema Waziri Mazrui
alifafanua kuwa Wizara yake imepokea Dawa 165 zenye thamani ya takribani
Shilingi Milioni 120 kwa Unguja ambazo ni idadi sawa na Dawa zilizotolewa
Kisiwani Pemba.
Kwa upande wake Balozi
Mdogo wa China anaefanyia kazi zake Zanzibar, Zhan Zhisheng amesema Serikali ya watu wa China
imedhamiria kuendelea kuisaidia Zanzibar kwani tayari wameshajaza mkataba wa
kujenga nyumba za wafanyakazi katika Hospitali ya Abdalla Mzee iliopo Mkoani
Pemba.
Hata hivyo Balozi Zhan
amefurahishwa na mashirikiano yaliyopo baina ya madaktari wa Zanzaibar na
madaktari kutoka China katika utendaji wa kazi unaopelekea kubadilishana
Ujuzi katika utekelezaji wa majukumu yao.
Makabidhiano hayo ya
Dawa baina ya Wizara ya Afya Zanzibar na Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China
yalifanyika katika Ukumbi wa mikutano Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Unguja.





0 Maoni