Klabu ya Al Ahly Nchini Misri imefikia makubaliano na Matajiri wa Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Simba SC juu ya uhamisho wa winga wake hatari Luis Jose Miquissone mzaliwa.

Miquissone mwenye Umri wa Miaka 26 Raia wa Msumbiji usajili wake utaigharimu Miamba hiyo ya Afrika ada ya uhamisho wa US$900,000 sawa na Shillingi za Kitanzania Bilioni 2.1 ambapo  atasaini mkataba wa miaka minne.