Waziri wa Afya,
Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui
(wa pili kushoto) akipokea moja ya vifaa vifaa tiba vitakavyotumika kwenye
kliniki inayotembea (Mobile clinic) kutoka kwa maofisa waandamizi wa benki ya
NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki
Masuke (wa pili kulia)wakati wa hafla hiyo iliyofanyika ofisini kwa
waziri huyo, Zanzibar. Vifaa hivyo vimetolewa benki hiyo kwa serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto
visiwani humo.Na mwandishi wetu
Benki ya Taifa ya Biashara NBC, imekabidhi msaada wa vifaa tiba ikiwemo UtraSound machine vitakavyotumika kwenye kliniki inayotembea (Mobile clinic) ambayo pia imetolewa na Benki hiyo kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto visiwani humo.
Akizungumza mara baada
ya kupokea vifaa hiyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh mil 19.5 jana Agosti
27, 2021, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na
Watoto Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui pamoja na kuishukuru benki hiyo kwa
msaada huo, alisema serikali hiyo itahakikisha msaada huo utatumika kama
ilivyokusudiwa.
“Msaada huu ni muhimu
na kiukweli unahitajika sana. Jukumu letu kama serikali ni kuhakikisha vifaa
hivi vinatunzwa na vinatumika kama ilivyokusudiwa ili vilete tija iliyolengwa
kwa maana visaidie haswa kuokoa maisha ya wazanzibar wakiwemo wakina mama na
watoto hasa walipo pembezoni.
Aliahidi kwa niaba ya
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuendeleza ushirikiano na Benki hiyo hususani
kwenye masuala mbalimbali ikiwemo yale yanayohusu ustawi wa jamii huku
akibainisha kuwa uimara wa Benki hiyo kwenye utoaji wa huduma zake visiwani
humo kwa kiasi kikubwa unachagizwa na namna inavyoshirikiana na jamii ya
Wazanzibar ikiwemo kibiashara na mambo ya kijamii.
“Naamini kabisa uimara
wa benki ya NBC tangu ilipoanza kutoa huduma zake hapa Zanzibar ni matokeo ya
ushirikiano iliyonayo na jamii ya Wazanzibar…nawapongeza sana na ninaomba
muendelee kuguswa zaidi,’’ aliongezea.
Mkurugenzi wa wateja
binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke (kulia) akisalimiana na
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto
Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui wakati wa makabidhiano hayo.Kwa upande wake Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki ya NBC Bw Elibariki Masuke alisema pamoja na msaada huo benki hiyo itaendelea kuhudumia vifaa hivyo hata pale vitakapokuwa vinapata hitirafu za kiufundi.
“Benki ya NBC tumekuwa
tukiguswa na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye huduma za afya hapa nchini
ikiwemo Zanzibar na ndio maana tumekuwa mstari wa mbele kuhakikisha
tunashirikiana na serikali zote mbili kukabiliana na changamoto zinazohusu
sekta hii muhimu.’’
“Tunaamini kupitia
vifaa hivi vitakavyofungwa ndani ya kliniki inayojongea wataalamu wa afya
wataweza kuwafikia walengwa popote walipo hususani wale waliopo pembezoni
wakiwemo wakina mama na watoto na kupitia msaada wa Mungu tutaweza kuokoa
maisha yao,’’ aliongeza.
Akizungumzia msaada
huo Mratibu wa Huduma ya Afya ya Uzazi na Mtoto, Wizara ya Afya Zanzibar Bi
Wanu Bakari alisema msaada huo umefika wakati muafaka wakati serikali hiyo
ikipambana kusogeza huduma za afya hususani maeneo ya pembezoni ili kuepukana
na changamoto ya vifo vya akina mama na watoto wakati wa kujifungua.
“Tunaishukuru sana
benki ya NBC kwa kuliona hili na kwa kweli wametugusa sana! Kwa mfano kupitia
kliniki hii tutaweza kutoa huduma ya Utrasound ambapo kwa kwasasa
tunakabiliwa na uhaba wa huduma hii hivyo tatizo linakwenda kupungua. Zaidi pia
miongoni mwa vifaa hivi pia vipo vifaa vya uchunguzi wa afya za kina mama
wajawazito kitu ambacho kitatusaidia kuwafanyia uchunguzi kwa haraa pale
itakapohitajika kabla hawajapata madhara zaidi,’’ aliongezea.
Waziri wa Afya,
Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed
Nassor Mazrui (alieketi) akizungumza na maofisa waandamizi wa benki ya NBC
wakiongozwa na Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki
Masuke (kushoto) wakati wa makabidhiano ya vifaa hiyo yaliyofanyika ofisini
kwa waziri huyo Zanzibar. Wengine ni pamoja na Meneja wa benki ya NBC
tawi la Zanzibar Bw Ramadhani Lesso (Kulia) na Mkuu wa Idara ya Huduma za
Kiislam wa Benki hiyo Mohamed Nuh
Mkurugenzi wa wateja
binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke akisaini kitabu cha wageni
alipoingia kwenye ofisi ya Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee
Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed Nassor Mazrui wakati wa makabidhiano hayo.
Meneja wa benki ya NBC
tawi la Zanzibar Bw Ramadhani Lesso (Kulia) akisalimiana na Waziri
wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed
Nassor Mazrui wakati wa makabidhiano hayo.



0 Maoni