Aliyewahi kuwa Waziri wa Fedha wa Tanzania, Basil Pesambili Mramba amefariki dunia leo katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.

Mtoto wa Marehemu Mramba, Godfrey Mramba imesema baba yake amekutwa na umauti leo asubuhi wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Regency.

Hata hivyo, ameweka wazi kuwa kutokana na janga la Covid-19 ni wanafamilia wachache wataruhusiwa kufika kutoa pole nyumbani kwa marehemu, Mawenzi Road, Oysterbay Dar es Salaam.

Marehemu Mramba aliwahi kuwa Waziri wa Fedha katika utawala wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ambapo aliiongoza Wizara hiyo mwaka 2001-2005, baadaye Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko mwaka 2006 hadi 2008.