Baada ya Pambano la Ngumi kumalizika Jana (Agust 20) kati ya Dulla Mbabe na Twaha Kiduku kumalizika na hatimae Twaha Kiduku kushinda, Tambo za ushindi huo zikaamia mitandaoni
Kupitia mtandao wake wa Kijamii Mbunge wa Morogoro
Kusini Mashariki, Hamisi TaleTale 'Babu Tale' amesema yupo tayari kutoa gari
aina ya V8 2020 ili Bondia Twaha Kiduku wa Morogoro na Hassan Mwakinyo wa Tanga
wapande ulingoni kuzichapa.
Kauli ya Tale inakuja mara baada ya hapo Twaha
Kiduku kumchapa Dullah Mbabe kwa pointi na kuondoka na gari aina ya Toyota
Crown.
“Wapeni salaam Morogoro ndio mkoa pekee unaobeba
magari yenu yote ya Dar. Tanga eeeh kubalini basi tumalize hili jambo, naweka
V8 ya mwaka 2020. Oya Mwana FA mjuze mwanao basi. Asante Twaha Kiduku umetuheshimisha
wana Morogoro”amesema Babu Tale.
Mbunge wa Muheza Tanga nae alijibu suala hilo kwa kumtaka Babu Tale waandae pambano lenye mkanda.




0 Maoni