Na Mwandishi wetu

Mkuu  wa  Mkoawa  Kaskazini Unguja  Ayoub  Mohamed  Mahmoud  amewahimiza  wakazi wa Nungwi  kuendeleza  utamaduni wao  ili  kuwanusuru  Vijana  kujiingiza katika  mambo maovu.

Akifungua  mashindano  ya Qur-an  ya QAl-madrasatul-Rahma Qur-nia iliyopo  Nungwi  ikiwa  ni tathmini  ya uhifadhi  wa Qur-an  kipindi  cha  robo Mwaka  katika  Madrasa  hiyo  Mkuuwa Mkoa  Ayoub  amesema  kuwalea  watoto  katika  misingi  ya  Dini  ya  Kiislamu  ni  utamaduni  wa  Kizanzibar  hivyo  ni  wajibu  wa  jamii  kuhakikisha Watoto  wao wanakwenda  Madrasa.

Amesema utu wa  mtu  unatokana  na utamaduni  hivyo  kuwacha  utamaduni  wako  na kufuata  utamaduni wa  kigeni ni kiashiria  cha  kupoteza  utu .

Akisoma  risala  ya  Madrasa hiyo  Ostadh  Hamadi  Shehe  Makame amesema  ingawa wamefanikiwa  kuwahifadhisha Qur-an   Watoto  zaidi  ya mia nne  lakini  bado  Madrasa  inakabiliwa  na  upungufu  wa  Madarasa , vikalio, vyoo  pamoja  na  kukabiliwa  na mmomonyoko  wa maadili  kwa  wakazi  wa  Nungwi  jambo ambalo  linarejesha nyuma  jitihada  za  walimu  na  wazazi  za  kuwalea  watoto  katika  misingi  ya  dini.

Mwalimu  Mkuu  wa  Madrasa  hiyo Wadi  Makame   Silima  amemshukuru  Mkuu  wa  Mkoa  kwa  msaada  wa matofali na mchanga  kwa  ajili ya  ujenzi  wa  madrasa  yao  na  kuwataka  waislamu  wote  wa Nungwi  kuwasikiliza  viongozi  wa  Dini  na  Serikali  katika  mambo  ya  kheri  wanayo elekeza.