Mbunge wa Jimbo la Kawe Jijini Dar Es Salam na Askofu wa Kanisa Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema tayari ameshapokea barua ya wito wa kuitwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Jijini Dodoma.
Jana,katika mitandao mbalimbali ilisambaa mitandaoni ya barua ya ofisi ya
Bunge ikionyesha Gwajima na mbunge wa Ukonga, Jerry Slaa wanatakiwa kwenda
mbele ya kamati hiyo Agosti 23 na 24.
“Nimepokea barua ya Spika kwenda kwenye kamati,
nitakwenda. Nimesema hapa kwa kuwa aliyenitumia barua ameweka mitandaoni
akisema kwanini nimesema hapa na yeye aniambie kwa nini aliweka mitandaoni,”
amesema Gwajima leo, Agosti 22, 2021 alipokuwa akizungumza na waumini wake
katika kanisa hilo, Dare es Salaam.
Askofu Gwajima amesema atakwenda kwenye kamati
hiyo na atasimamia ukweli kama ambavyo imani yake inamtuma.
“Nitakwenda kwenye kamati wategemee ukweli
nitasema ukweli kwa kuwa imani ya CCM ni ukweli na nitaongeza mengine ambayo
sijawahi kusema. Lazima tusimamie nchi na watoto wa watoto wetu,” amesema
askofu Gwajima.
Tukio hilo linajiri baada ya hivi karibuni Spika
wa Bunge wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Job Ndugai kuwataka wabunge hao
kufika mbele ya kamati ya Maadili ya Bunge kwaajili ya kuhojiwa kuhusiana na
mambo ya Covid waliyokuwa wakiyazungumza





0 Maoni