Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akifurahia pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua jengo la madarasa ya Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akizungumza na mmoja wa
wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi (Kushoto) wakati akijiandaa
kuzindua jengo la madarasa ya skuli hiyo yaliyojengwa na kukarabatiwa kwa
msaada wa benki ya NBC wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika leo Kijiji
cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar. Wengine ni pamoja na
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee Jinsia na Watoto Zazibar, Ahmed Nassor
Mazrui (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria, Utumishi na
Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haroun Ali Suleiman (wa tatu
kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa pili kulia)
Wanafunzi wa Skuli
ya Maandalizi ya Kizimkazi wakitoa burudani mbele ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi waandamizi wa
serikali ya Mapinduzi Zanzibar , viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC)
pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.Monekano wa jengo la madarasa ya Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (katikati) akifurahi pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua Kliniki inayohamishika (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa serikali ya Mapinduzi ya Waziri wa Afya Ahmed Nassor Mazrui (wa pili kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba na Sheria, Haroun Ali Suleiman (Kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (wa tatu kushoto) na Mkurugenzi wa wateja binafsi wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke (Kushoto).
Baadhi ya wagenini waalikwa pamoja viongozi wa benki ya NBC wakifuatilia makabidhiano hayo.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Bw Theobald Sabi (kulia) akifafanua jambo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan wakati Rais alipokuwa akigagua jengo la madarasa ya Skuli ya Maandalizi ya Kizimkazi lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akijadili jambo na baadhi ya
viongozi waandamizi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar na viongozi wa
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) mara baada ya kuzindua Kliniki
inayohamishika (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto
visiwani humo wakati wa hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika leo Kijiji cha
Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
NBC Mambo poa! Ndivyo
wanavyoonekana wakisema baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Maandalizi ya
Kizimkazi walipohudhuria hafla ya makabidhiano ya jengo la madarasa ya Skuli
hiyo lililojengwa na kukarabatiwa kwa msaada wa benki ya NBC.Wanafunzi na wakazi wa Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar wakiwa wameketi pembeni ya Kliniki inayohamishika (mobile Clinic) iliyotolewa na Benki ya NBC kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuboresha huduma ya afya hususani ya mama na mtoto visiwani humo wakati wa hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo Kijiji cha Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar











0 Maoni