Jeshi la Polisi  Mkoani Manyara  linamshikilia Mwanaume Mmoja ajulikanae kwa jina la Harod Hhando  Mkazi wa Mtaa wa Silaloda Mji wa Mbulu Mkoani Manyara, kwa tuhuma za kumuua mtoto wa kaka yake, Emmanuela Hhando (13) na kumtoa viungo vya mwili.

Taarifa yake aliyoitoa kwa njia ya Simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Marrison Mwakyoma amesema Hhando anahusishwa na mauaji ya  mtoto huyo kwa kumpasua katikati ya miguu na kumtenganisha vipande viwili kisha kukata sehemu za siri, kumtoa maini na kutaka kuyapika kama mboga kwaajili ya kula.

Kamanda Mwakyoma amesema tukio hilo lilitokea juzi August 21,2021 katika kijijinicha Silaloda .

Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha tukio hilo ni imani za ushirikina baada ya Hhando kuelezwa na anaedaiwa kuwa ni mungu wake amuue mtoto wa kaka yake na kula maini ili avune mazao mengi.