Hivi karibuni Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DR Hussein Ally Mwinyi alifanya ziara katika Wilaya zote za Unguja na katika ziara hizo yapo madudu kadhaa aliyoeleza kuyabaini katika kila Halmashauri.
Wakati anafanya majumuisho ya ziara hiyo akiwa ndani ya Mkoa wa
Mjini Magharib Raisi alieleza kusikitishwa na kitendo cha Mabaraza ya Mji /Manspaa
Kutumia kiwango kikubwa cha pesa walizokusanya kwa wananchi kama sehemu ya Kodi kwa Halmashauri hizo kutumika katika shughuli za
kawaida huku fedha chake pekee ndo
hupeleka katika shuhuli za maendeleo kwa Wananchi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Hamad Mbwana Shehe pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mohammed Mussa Mkobani wakawashauri madiwani hao kushirikiana kusimamia ukusanyaji wa mapato
Mapema akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Ramadhan Nyerere Tosha amewataka madiwani kuendelea kuibua vyanzo vipya vya mapato ili kuongeza mapato ya Halmashauri.




0 Maoni