Makamu wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla alieleza hayo Ofisini kwake Vuga Jijini
Zanzibar wakati akipokea Stakabadhi ya msaada huo wa chanjo kutoka kwa Balozi
Mdogo wa China anaefanyia kazi zake Zanzibar Bwana Zhang Zhisheng
Mhe. Hemed alisema
chanjo hizo aina ya SINOVAC zinategemewa kuwasili Zanzibar
ndani ya muda mfupi baada ya kupokea Stakabadhi na mara baada ya kuwasili
Zanzibar zinatakibidhiwa kwa Wizara ya Afya ikiwa ndio wizara yenye dhamana na
musuala ya Afya.
Alisema Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar itapokea chanjo hizo, ikiwa ni katika juhudi za kujikinga
na Maradhi ya Covid 19, kwa lengo la kuwakinga wananchi wake kutokana na virusi
vinavyosababisha maradhi hayo.
Akizungumzia Ubora wa
chanjo hiyo Makamu wa Pili wa Rais aliwahakikishia wananchi wa Zanzibar kuwa
chanjo hiyo ni salama kwani imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa
ajili ya matumizi.
Katika hatua nyengine
Mhe. Hemed aliendelea kuishukuru Serikali ya Jamhuri ya watu wa China kwa
kuendelea kuunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa katika Sekta ya
Afya, akitolea mfano misaada mbali mbali inayotolewa na Nchi hiyo katika
Hospitali na Mnazi Mmoja na ya Hospital ya Abdallah Mzee kwa Upande wa Pemba.
Alifafanua kuwa,
mashirikiano hayo yanaonesha ukaribu na udugu kati ya nchi hizo mbili
yaliyoasisiwa kwa muda mrefu sasa ambapo hadi sasa China na Zanzibar
zinashirikiana kupitia sekta tofauti.
Nae Balozi Mdogo wa China Bwana Zhang Zhisheng alisema China imejipanga kutoa chanjo ili kusaidia kinga dhidi ya covid 19 na alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa chanjo hizo ni salama kutokana na kupatikana kwa ruhusa ya kimatumizi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO).
Aidha, Bwana Zhang
Zhisheng alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kuwa Nchi ya
China itaendeleza mashirikiano yaliyopo baina yao ili kuisaidia Zanzibar
kukuza uchumi wake ambapo serikali ya Jamuhuri ya watu wa China imejipanga
kuisaidia Zanzibar katika kuwekeza kwenye Sekta ya Viwanda jambo ambalo
litasadia kuinua uchumi wa zanzibar na watu wake.





0 Maoni