Klabu ya Yanga rasmi imeingia Makubaliano ya Mkataba
na Azam Media ya Mashirikiano ya Maudhui,mkataba ambao wenye Thamani ya Shilingi Bilioni 41 pamoja na
VAT kwa Kipindi cha Miaka 10(sawa na bilioni 34.8 bila VAT)
Hafla ya Makubaliano hayo yamefanyika katika Hoteli
ya Serena Jijin Dar Es Salam asubuh ya Tarehe 8 mwezi July Mwaka 2021 ambapo
Azam Media waliwakilishwa na Tido Mhando
ambae ni Afisa mtendaji Mkuu wa Azam Media na Klabu ya Yanga iliwakilishwa na Dr Mshindo
Msolla ,ambae ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo.
Mkataba huo wa miaka Kumi(10) itaiwezesha Klabu ya
yanga katika Mwaka wa Kwanza kujikusanyia kila mwezi kutoka kwa Azam Media kiasi
cha Shilingi Milioni Mia Mbilim za Kitanzania na Mwaka unaofuata itaongezeka
Milioni Ishirini (20)
Mkataba huo pia umeipa nafasi yanga kujikusanyia
bonas hadi shilingo Bilioni Tatu ikiwa kwa Kuanzia Msimu ujao Klabu hiyo Kongwe
Barani Afrika itamaliza Msimu ikiwa katika nafasi mbili za Juu.
Klabu ya Yanga Afrika imetengeneza Rekodi nyengine hii leo na kua klabu ya Kwanza
Tanzania Kumiliki chaneli yake na Sio kipindi cha Dakika 30 kama ilivyo kwa
Mahasimu wao Simba.
Ikumbukwe Yanga hivi Karibuni walifanya Mkatano Mkuu ambao sambamba na mambo mengine wanachama wa klabu hiyo walipitisha kwa Kauli Moja Ajenga ya Mabadiliko ya kikatiba ambayo itaiwezesha Yanga kuruhusu wawekezaji kwaajili ya Uwekezaji Mkubwa utakaoleta Faida kwa wanachama na Clabu kwa Ujumla
Mkataba huo unaweza kusema sasa Rasmi Yanga watakua wamewaacha mbali watani wao wa Jadi Simba kwakua bado Mkataba huo wa haki za maudhui haujawafikia.






0 Maoni