Zanzibar

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Smz amewataka watendani walio chini ya Wizara hiyo kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

 Amesema hayo wakati akizungumza na watendaji wa Wizara hiyo ikiwemo Madiwani wa Mkoa Mjini Magharibi amesema kumekua na Changamoto za kiutendaji ambazo taarifa zake hazifiki kwa Viongozi wa Juu jambo ambalo linachangia kurudisha nyuma ufanisi na kupelekea uwepo wa mchanganyiko wa Taarifa kwa Jamii.

 Mh Masood amesema Serikali imefanya mabadiliko  kwa wasimamizi katika Masoko ya Mkoa wa Mjini ikiwemo Mwanakwerekwe na Shimoni lengo la mabadiliko hayo ni kuleta ufanishi wa utendaji kazi na sio kuwakoa wengine.

 Katika hatua nyengine Mh Masood amewataka madiwani kuanda Siku na muda maalumu kwa ajili ya kusikiliza kero za wanachi ili kupunguza mrundikano wa wananchi kupeleka Malalamiko katika ofisi za Mkuu wa Mkoa na Wilaya.

 Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mgharibi amepongeza juhudi wa Waziri huyo katika Maamuzi ya kuboresha Usimamizi katika masoko huku akiahidi kusimamia fedha makusanyo ili kuongeza Mapato Serikalini,