Takribani watu elfu tatu wanapoteza maisha nchini Tanzania kutokana na ajali za kuzama majini kwa mwaka

 Mkurugenzi mtendaji wa shirika la usimamizi wa mazingira na maendeleo EMEDO, Editrudith Lukanga amesema vifo vya maji vimekuwa vikiua lakini havizungumzwi.

 Ameeleza kuwa kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO vifo vya maji ni asilimia 7 ya vifo vyote duniani na hiyo ndiyo sababu wameandaa maadhimisho ya siku maalum ya kuzuia kuzama maji itakayoadhimishwa kwa mara ya kwanza kesho Julai 25 katika fukwe za Kunduchi.

 Takwimu zinaonyesha watu laki mbili na 36 elfu hupoteza maisha kutokana na ajali za maji Duniani ambapo zaidi ya asilimia 90 ya vifo hivyo, hutokea katika nchi zenye kipato cha chini na zile zenye uchumi wa kati.