Imeripotiwa kuwa watu wasiopungua 800 katika nchi ya Uganda iliyoko Afrika Mashariki walipewa chanjo ya bandia dhidi ya virusi vya corona (Kovid-19).
Mkuu wa Kitengo cha
Ufuatiliaji wa Afya, Dk. Wallen Naamara, katika taarifa yake, alisema kuwa kesi
za maambukizi ya Kovid-19 zinazoongezeka kila siku nchini zinatia wasiwasi.
Naamara alieleza,
"Watu wengine wasio
waaminifu kwa nia ya kupata pesa nchini walidanganya umma katika zoezi la
chanjo ya bandia ya Kovid-19."
Akibainisha kuwa angalau
watu 800 walipewa chanjo ya bandia kati ya Mei na Juni nchini, Naamara alisema
kuwa watu wengine walipewa maji badala ya chanjo.
Naamara pia alisema kuwa
wauguzi wawili walizuiliwa katika uchunguzi uliozinduliwa juu ya tukio hilo, na
daktari mhusika alikuwa akitoroka.
Akisisitiza kwamba
chanjo ya Kovid-19 ni bure nchini, Naamara alitoa wito kwa umma kukaa mbali na
chanjo hizo za kulipia.





0 Maoni