Hayo yamesemwa leo na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo wakati akizungumza
na wananchi wa Kijiji hicho kwenye Mkutano wa Hadhara wakati wa ziara yake
yakuendelea kuskiliza Changamoto mbali mbali zinazowakabili wananchi
Amwataka wananchi hao
kuungana na Serikali katika kuhakikisha wale wote wanaojihusishwa na matukio ya
Uuzaji na utumiaji wa dawa za kulevya,matendo ya udhalilishaji,uporaji na wizi
wanaripotiwa katika vyombo vya Sheria.
“Kuna wengine wamesema
yapo matukio ya kihalifu hapa yanafanyika, watu wanaiba hapa, watu wanatembea
uchi, bangi zinauzwa hapa, sasa akitokea mtu anatokea sehemu ya mbali kama
mlivyosema anafanya matendo ya uhalifu basi mripoti kwa Jeshi la
Polisi,mkishajua huyu ndio muuza unga maarufu hata mimi niambieni nitawatuma
askari wangu waje wamshughulikie,msimpige wala msichukue sheria mkononi
chukueni hatua za kinidhamu na kisheria sio mumpige mtakuja kutengeneza balaa
linguine” alisema Naibu Waziri Chilo
Awali mkazi wa Kijiji
hicho Said Mpangaleni akizungumza katika mkutano huo amesema kuwepo kwa
uhalifu uliokithiri katika Kijiji chao imepelekea kudumaa kwa shughuli za
kimaendeleo watu wakihofia usalama wao
“Hapa kuna genge la
uuzaji na utumiaji dawa za kulevya na ndio linaratibu uhalifu wote katika
Kijiji hiki,mtu akishakula maunga yake kinachofatia ni uhalifu tu kwa kweli
tumekua tukiishi kwa hofu,bora sisi wanaume tuna afadhali lakini dada zetu
wanaporwa mchana kweupe,Serikali itusaidie kwenye hili kwani kwa hali hii huo
uchumi tunaoambiwa hatuwezi kuupata hali huku ni tete” alisema Said
Wakitoa neno la
shukrani baada ya mkutano huo wawakilishi wa wananchi hao wameiomba serikali
kufungua kituo cha polisi katika maeneo hayo kwani itarahisisha udhibiti wa
uhalifu katika Kijiji chao hali itakayopelekea kustawi kwa amani huku pia
wakiomba kuongezwa kwa askari wa ulinzi shirikishi.





0 Maoni