wanajeshi sita wa Cameroon wameuwawa Jumamosi katika shambulio lililotekelezwa na Wanamgambo wa Boko Haram kaskazini kabisa mwa nchi hiyo.
Kupitia Runinga ya
Serikali Gavana wa Mkoa huo amesema licha ya tukio hilo lakini wanajeshi wa
Serikali bado wanaendelea kupambana.
Boko Haram walifanya
shambulio kwenye kituo cha jeshi huko Sagme, karibu na mpaka na Nigeria,
kaskazini kabisa mwa nchi hiyo Jumamosi asubuhi. Eneo ambalo Boko Haram imekuwa
ikitekeleza mara kwa mara mashambulizi.





0 Maoni