Zanzibar
Waziri wa Afya Ustawi
wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui amesema serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kuwapatia chanjo ya Covid 19 wafanyakazi wa
sekta ya Utalii ili kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa amani na usalama
Waziri Mazrui
ameyasema hayo Ofisini kwake Mnazi Mmoja wakati alipotembelewa na Balozi wa
Umoja wa Nchi za Ulaya Mnafredo Fanti pamoja na Ujumbe wake kwa ajili ya
kujitambulisha, amesema sekta ya utalii ni sekta muhimu nchini katika kukuza
uchumi ni vyema wafanyakazi wake wakapata kinga ya kujikinga afya zao dhidi ya
maambukizi ya Corona na kufanyakazi kwa amani.
Amesema serikali
itaanza na sekta hiyo kutokana na wafanyakazi wake kukutana na mchangamyiko wa
watu mbalimbali na kuthibisha usalama wa wageni wanapoingia kwa watendaji wake
“Tunaanza kwa
wafanyakazi hao kuapatiwa Chanjo ili kuzithibitishia nchi zinazoleta Watalii
kuwa Zanzibar ni nchi salama kwa ajili ya shughuli mbalimbali za
kiutatalii”, alieleza Waziri huyo
Amefahamisha kuwa
watakaopatiwa chanjo hiyo ni pamoja na wafanyakazi wa hoteli, watendaji
wa Viwanja vya Ndege, waongozaji watalii ili kufanyakazi kwa ufanisi na
usalama.
Kwa upande wake Balozi
wa Umoja wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fant amesema ana matumaini
makubwa na ameahidi kushirikianana na Zanzibar katika kupambanana
ugonjwa wa Covid-19 ambao ni janga lililoikumba Dunia nzima.
Hata hivyo amesema
kuwa Umoja huo utakuza mashirikiano zaidi ya kuisaidia Zanzibar katika
nyanja mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo Afya, Kijamii, na kiuchumi.
ANGALIA TUKIO ZIMA HAPA CHINI MAELEZO NA PICHA KILE ALICHOKISEMA WAZIRI WAFANYAKAZI MAHOTEL KUPATIWA CHANJO





0 Maoni