Zanzibar
Mufti Mkuu wa
Zanzibar, Sheikh, Saleh Omar Kaabi, amewataka viongozi wa Dini, na Masheha
kuendelea kuhubiri amani kwa mujibu wa nafasi zao ili Nchi iendelee kuwa na
Amani
Akizungumza katika mkutano wenye lengo la kudumisha amani ya Nchi uliowashirikisha Maimamu, Walimu wa Madrasa na Masheha wa Wilaya ya Magharibi ‘A, na ‘B’ Uliyofanyika katika Ukumbi wa Msikiti wa Jamii Zanzibar ulioko Mazizini nje kidogo na Mji wa Zanzibar.
Amesema imani ya Dini ya Kiislamu inahitaji kuendelezwa, hivyo ipo haja kwa viongozi hao kuendelea kutoa taalamu katika misitiki, Madrasa na Shehia zao ili kudumisha madili na heshima ya Kizanzibar.
Amefahamisha kuwa msingi wa Dini ya Kiislamu ni kuendeleza amani kwa Mataifa mbalimbali hivyo ni vyema viongozi hao kuendelea kuhubiri amani na kuendelea kuwajaza waumini wao imani ya kweli.
Aidha amesema ni vyema viongozi hao kuendelea kushirikiana na viongozi wa Nchi sambamba na kuwaombea dua katika sala zao hasa katika sala ya Ijumaa jambo ambalo sio zambi kulifanya.
Akizungumzia vitendo vya udhalilishaji ambapo kwa sasa vimeshika kasi katika nchi, ikiwemo kwa Walimu wa Madrasa, Mufti Kaabi, amesema Ofisi yake, inatarajia kuandaa mpango maalum wa kuwafanyia uhakiki Maimamu na Walimu wa madrasa ili kujua tabia zao na kiwango chao cha elimu ili kuendana na elimu wanayoitoa kwa waamini.
Amesema hatua hiyo, itasaidia kuondosha walimu ambao hawana vigezo na hujiingiza katika vitendo vya udhalilishaji kwa wanafunzi.
Nae Katibu wa Mufti Zanzibar, shekh Khalid Ali Mfaume, amesema kuendeleza kwa vitendo vya udhalilishaji ndani ya taasisi za dini ni kuitia doa dini na viongozi hao kutoaminiwa na wananchi.
Kwa upande wa Mashehe, Katibu Khalid, aliwataka kutokubali kuruhusu ujenzi wa misikiti katika Shehia za hadi wapate kibao kutoka ofisi ya Mufti ili kuweza kuepusha misikiti kujaa katika shehia moja huku shehia nyengine zikiwa zinahitaji.
Nao washiriki wa mkutano huo wamewataka maimamu kubadilika katika kutoa hutuba zitakazoendana na matukio yanayotokea katika jamii na kuweza kuondoka. amewataka viongozi wa Dini, na Masheha kuendelea kuhubiri amani kwa mujibu wa nafasi zao ili Nchi iendelee kuwa na Amani
Akizungumza katika mkutano wenye lengo la kudumisha amani ya Nchi uliowashirikisha Maimamu, Walimu wa Madrasa na Masheha wa Wilaya ya Magharibi ‘A, na ‘B’ Uliyofanyika katika Ukumbi wa Msikiti wa Jamii Zanzibar ulioko Mazizini nje kidogo na Mji wa Zanzibar.
Amesema imani ya Dini ya Kiislamu inahitaji kuendelezwa, hivyo ipo haja kwa viongozi hao kuendelea kutoa taalamu katika misitiki, Madrasa na Shehia zao ili kudumisha madili na heshima ya Kizanzibar.
Amefahamisha kuwa msingi wa Dini ya Kiislamu ni kuendeleza amani kwa Mataifa mbalimbali hivyo ni vyema viongozi hao kuendelea kuhubiri amani na kuendelea kuwajaza waumini wao imani ya kweli.
Aidha amesema ni vyema viongozi hao kuendelea kushirikiana na viongozi wa Nchi sambamba na kuwaombea dua katika sala zao hasa katika sala ya Ijumaa jambo ambalo sio zambi kulifanya.
Akizungumzia vitendo vya udhalilishaji ambapo kwa sasa vimeshika kasi katika nchi, ikiwemo kwa Walimu wa Madrasa, Mufti Kaabi, amesema Ofisi yake, inatarajia kuandaa mpango maalum wa kuwafanyia uhakiki Maimamu na Walimu wa madrasa ili kujua tabia zao na kiwango chao cha elimu ili kuendana na elimu wanayoitoa kwa waamini.
Amesema hatua hiyo, itasaidia kuondosha walimu ambao hawana vigezo na hujiingiza katika vitendo vya udhalilishaji kwa wanafunzi.
Nae Katibu wa Mufti Zanzibar, shekh Khalid Ali Mfaume, amesema kuendeleza kwa vitendo vya udhalilishaji ndani ya taasisi za dini ni kuitia doa dini na viongozi hao kutoaminiwa na wananchi.
Kwa upande wa Mashehe, Katibu Khalid, aliwataka kutokubali kuruhusu ujenzi wa misikiti katika Shehia za hadi wapate kibao kutoka ofisi ya Mufti ili kuweza kuepusha misikiti kujaa katika shehia moja huku shehia nyengine zikiwa zinahitaji.
Nao washiriki wa mkutano huo wamewataka maimamu kubadilika katika kutoa hutuba zitakazoendana na matukio yanayotokea katika jamii na kuweza kuondoka.

0 Maoni