Mwakilishi kutoka Taasisi ya Umoja wa Falme za
Kiarabu Shekh Ahmed Al- Falasi ameahidi kushirikiana na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar kujenga Hospitali zitakazotoa huduma muhimu kwa jamii
ili kuimarisha sekta ya afya nchini.
Ameyasema hayo wakati Akizungumza na Waziri wa
Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto Mh Nassor Ahmed Mazrui ofisini
kwake Vuga Jijini Zanzibar.
Shehe Ahmed amesema taasisi hiyo imekusudia
kujenga hospitali za kisasa Unguja na Pemba zitakazokua zikitoa huduma Muhimu
sambamba na kusaidia vifaa tiba katika hospitali kuu za
Zanzibar .
Nae Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee,
Jinsia na Watoto Nassor Ahmed Mazrui ameipongeza Taasisi ya Umoja
wa Falme za Kiarabu kwa kuiunga mkono na kuisadia Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar yenye lengo la kuimarisha sekta ya afya nchini.
“Huduma za afya zikiimarishwa kwa
wananchi zitasaidia kuondoa usumbu uliopo na kutoa huduma nzuri kwa kijamii na
kuleta kimaendeleo nchini”, alifahamisha Waziri Mazrui .
Waziri huyo alieleza kuwa pia taasisi hiyo
inalengo la kuzisadia hospitali kuu za Unguja na Pemba kwa kuzipatia vifaa ili
zipate kutoa huduma bora kwa wananchi na kuondosha usumbufu uliopo nchini
.




0 Maoni