Karibu wiki ya Pili sasa bado maeneo mbali mbali ya Tanzania Mjadala Mkubwa unaojadiliwa ni kuhusiana na Sheria Mpya ya Tozo katika simu.

Viongozi mbali mbali wamekua wakitolea ufafanuzi hilo lakini hata Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hasan alilizungumzia na kuitaka wizara kutafakari malalamiko ya wananchi

Sheia hii kama ilivyo kawaida imejadiliwa na kupitishwa na Bunge,hivyo wengi wakatamani kujua Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Job Ndugai anasemaje katika hili

Kufuatia hilo Spika Ndugai kwaupande wake amepigilia msumari kwenye tozo ya miamala katika simu kwa kudai Bunge ndio limepitisha na wale ambao wanapinga wanatakiwa kutoa mawazo mbadala nini kifanyike.

Amesema Lengo la Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ifikapo Mwaka 2025 Tanzania Iwe Nchi ya Mfano katika suala la Maendeleo ikiwemo Miundombinu ya Barabara,Afya na Maji

 Akizungumza leo, Julai 23, 2021, katika kikao kazi kilichoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, amesema wao kama Bunge ndio wameamua kuwe na tozo katika miamala ya simu kwa sababu fedha zitakakazopatikana zitaenda katika mfuko Maalum ambao utawasaidia wananchi.

"Tumepitisha sisi, tukatunga sheria sisi, tunataka kuliona hilo, sasa wewe ambaye unapinga tupe njia mbadala tutapata wapi fedha, tunafikaje 2025, kwa hiyo maamuzi ni hayo tumeyafanya, kwa nia njema kabisa kwamba 2025 tuwe tumetoka, tuwe ni taifa la Tanzania ambalo ni tofauti... CCM hoyee, nimemaliza

Spika Ndugai ameyazungumza hayo kufuatia baadhi ya wananchi kulalamika kwamba kumekuwa na tozo kubwa katika miamala ya simu.