Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuyashughulia malalamiko yote yanayotolewa na Watanzania kuhusu tozo mpya za miamala ya simu zilizoanza kutumika Julai 15/2021.
Akitoa tamko la Serikali kuhusiana na tozo hiyo
mpya, Waziri wa fedha na mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Samia
ameguswa na jambo hilo na kuagiza kufanyiwa kazi.
Ameeleza kuwa kikao cha ngazi ya juu cha kupitia
upya jambo hilo kitafanyika kesho na kitakuwa chini ya Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa.
Hata hivyo, amesema kwa kuwa jambo hilo ni la
kisheria zilizopitishwa na Bunge, utekelezaji wake utakuwa kwenye kanuni huku
akisisitiza sheria ziheshimiwe.
Aidha Dkt. Mwigulu amewaonya watu wanaopotosha
kuhusu jambo hilo na kuwataka wananchi kuwa watulivu.
Nae Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,
Dkt. Faustine Ndugulile amesema Wizara yake imekuwa ikikusanya maoni kuhusu
tozo hizo na itayafanyia kazi.
Ambapo ameahidi kumpa ushirikiano mkubwa Waziri wa
Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba kuhakikisha suala hilo linapatiwa
suluhu.





0 Maoni