Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Anna Mghwira kilichotokea leo tarehe 22 Julai, 2021 katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru mkoani Arusha alipokuwa akipatiwa matibabu.
Anna Mgwira aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, na mgombea urais kupitia chama cha ACT-Wazalendo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
Mama Anna Elisha Mghwira, amefariki dunia leo wakati akipatiwa matibabu
katika Hospitali ya Mount Meru, Arusha.
Imeelezwa kuwa Mama Mghwira amefariki dunia leo Julai 22,
2021, majira ya mchana, ambapo taarifa zinadai kwamba wiki moja iliyopita
alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo
baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru hadi umauti ulipomkuta.
Mh Anna Mgwira aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na Mwenyekiti wa Chama cha Act






0 Maoni