1. Amemteua Bwana Rogatus Hussein Mativila kuwa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).
Bwana Mativila anachukua nafasi ya Marehemu Mhandisi Patrick Mfugale
ambaye alifariki dunia tarehe 29 Juni, 2021.
Kabla ya uteuzi huo Bwana Mativila alikuwa Mkurugenzi wa Barabara, Wizara
ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).
2. Amemteua Prof. Yunus Daud Mgaya kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Kabla ya uteuzi huo Prof. Mgaya alikuwa Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu.
Uteuzi huo umeanza tarehe 28
Julai, 2021.





0 Maoni