RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameupongeza utayari wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza Tony Blair wa kuiunga mkono Zanzibar kupitia taasisi yake ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change).
Rais Dk. Mwinyi
aliyasema hayo leo Ikulu Jijini Zanzibar wakati alipokutana na kufanya mazungumzo
na Waziri Mstaafu huyo wa Uingereza Tony Blair ambaye alikuwepo Zanzibar kwa
ziara maalum ya siku moja.
Katika maelezo
yake, Rais Dk. Mwinyi alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanziba iko tayari
kushirikiana na Taasisi ya Waziri Mkuu huyo Mstaafu wa Uingereza ili uihakikisha
azma iliyokusudiwa inafikiwa.
Rais Dk. Mwinyi
alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri huyo Mstaafu wa Uingerza kwa kufanya
ziara Zanzibar na kuweza kubanilishana mawazo katika mustakbali mzima wa kuiletea
maendeleo Zanzibar.
Alieleza kwamba
ana matumaini makubwa kuwa mazungumzo baina yao yatakuwa chachu ya maendeleo
hasa ikizingatiwa kwamba Tony Balair ni kiongozi wmenye mwenye uzoefu mkubwa wa
uongozi duniani.
Hivyo Rais Dk.
Mwinyi alitoa shukurani zake kwa Waziri Mkuu huyo Mstafu na kueleza kwamba nia
yake njema ya kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Taasisi
yake ya Mabadiliko Ulimwenguni (Tony Blair Institute for Global Change) itaweza
kuleta manufaa makubwa ya kimaendeleo.
Aidha, Rais Dk.
Mwinyi alimueleza Waziri Mkuu huyo juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Awamu ya Nane katika kutekeleza mikakati, mipango na dira
zilizowekwa na Serikali ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kuiletea
Zanzibar maendeleo endelevu.
Nae Waziri Mkuu
Mstaafu wa Uingereza Tony Blair alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba Taasisi yake
iko tayari kushirikiana na kuiunga mkono Zanzibar katika kutafuta njia bora za
kupanga mikakati ya kutekeleza mipango ya maendeleo.
Tony Balair
alieleza kwamba timu yake kutoka Taasisi anayoiongoza iko tayari kuja na kukaa
na wataalamu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kuanza taratibu hizo za kuhakikisha
utekelezaji wa mazung mzo hayo unafanyika ikiwa ni pamoja na kusaidia vipaumbele
vya Serikali.
Waziri Mkuu huyo
Mstaafu alisema kuwa Taasisi yake inathamini sana juhudi zinazochukuliwa na
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Dk. Hussein Mwinyi
na kuahidi kwamba itakuwa bega kwa bega katika kuhakikisha inashiriki ipasavyo
kufikia malengo yaliyowekwa na Serikali.
Katika
mazungumzo hayo, Tony Blair alimueleza Rais Dk. Mwinyi kwamba Taasisi yake imekuwa
ikifanya kazi katika nchi mbali mbali katika Bara la Afrika hivyo, kushirikiana
na kufanya kazi na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutaweza kupanua wigo wamaendeleo.
Sambamba na
hayo, Waziri Mkuu huyo Mstaafu aliyasifu amzingira mazuri ya Zanzibar na
kuahidi kurudi tena kuja kuitembelea zaidi Zanzibar mara baada ya kumazika kwa janga
la maradhi ya COVID 19 duniani ambalo limemnyima fursa ya kutekeleza azma yake
hiyo kwa hivi sasa.




0 Maoni