JUMLA ya Ng’ombe ishirini wamekabidhiwa kwa jimbo la Kojani ,ili wananchi wapate kufurahia vyema Skukuu ya Iddi l-hajji, kama sadaka.
Akikabidhi msaada huo, Mbunge wa Jimbo hilo, Mh. Hamad Hassan Chande, amesema kila wananchi anatakiwa kufurahia skukuu ya iddi huku akiwataka wananchi kuongeza imani kwa Serikali ambayo inawahudumia kutatua changamoto zinazowakabili.
Akitoa shukurani baada ya kupokea sadaka hiyo , Mbunge wa jimbo la Pandani Mh. Maryam Said Omar, amesema sadaka hiyo imewafikia wakati ambao wananchi wanaohitaji.
Nao wananchi waliobahatika kupata sadaka hiyo wamesema, wameipokea sadaka hiyo na kuwataka wenye uwezo kuendelea kutoa kwa watu wasiokua na uwezo ,ili kueka furaha na umoja katika jamii hasa wakati wa skukuu.
Kiasi ya Ng’ombe miambili kisiwani Pemba, wametolewa kwa ushirikiano mkubwa wa Serikali kupitia ufadhili wa mradi wa dhulhijja pamoja na ushirikiano wa Arahma foundation ya Dar-es Salam na Dia net kutoka uturuki.





0 Maoni