MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Kaskazini Pemba, Asiya Sharif Omar, ameitaka jamii kutambua kuwa watoto wenye ulemavu bado wanahitaji kuthaminiwa pamoja na kupatiwa misaada yote kama wanavyopatiwa watoto wasio na ulemavu nchini.

Amesema ulemavu wao isiwe ni chanzo cha kukosa thamani kwa jamii, pamoja na kutokupatiwa haki zao stahiki ikiwemo suala zima la elimu, afya na huduma muhimu za kijamii.

Mbunge Asiya ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi misada mbali mbali kwa watoto wenye ulemavu, ikiwemo baskeli, taulo za kike, mchele na fedha taslimu huko Ungi Msuka Wilaya ya Micheweni.

Amesema utoaji wa msada huo ni utekelezaji wa ulani ya CCM, kwani CCM haina ubaguzi katika suala zima la kuwapatia wananchi wake maendeleo.

Naye mwakilishi wa jimbo la Konde Zawadi Amour Nassor, amesema msaada huo umekuja kwa wakati muwafaka, kwani watoto hao wamekuwa pata tabu wanapohitaji kutembea.

Aidha amepongeza uongozi wa UWT kwa juhudi zake mbali mbali wanazozichukua katika kuhakikisha wanawake wanafaidika kupitia miradi wanayoianzisha katika maeneo yao.

Nao wazazi wa watoto hao, wamemshukuru mbunge huyo kwa kutekeleza ahadi zake kwa vitendo na kuwasaidia watoto hao kuwapatia vibaskeli, ambavyo vitawasaida katika kutembea.

ANGALIA TUKIO ZIMA HAPA CHINI