Ikiwa kesho Waislam Duniani kote wanaungana katika kusheherekea sikukuu kubwa ya Kidini ya Eid El Haj viongozi mbali mbali kupitia mitandao ya kijamii wameonekana wakirusha Jumbe mbali mbali za kuwatakia Kheri na fanaka wananchi wao katika siku hiyo Muhimu.
Kupitia mitandao ya kijamii Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe Asia Sharif Omar amewatakia Kheri ya Sikukuu
Waislam wote na Watanzania kwa ujumla.
Katika Ujumbe wake wapili amewataka wazazi
kuhakikisha wanakua wakini na watoto wao hasa wanapokwenda katika kumbi za
skukuu ili kuwaepusha Watoto kutofanyiwa vitendo vya udhalilishaji
"Naendelea kuwahimiza wakinamama katika
kusheherekea skukuu hii wahakikishe wanakua makini na Watoto wao wanapokwenda
kwenye maeneo ya skukuu ili kumuepusha mtoto asifanyiwe vitendo vya
udhalilishaji. Tunaamini Zanzibar bila ya udhalilishaji inawezekan"
Skukuu ya Eid El Haj au Eid al-Adha maana yake ni "sikukuu
ya kutoa kafara/kuchinja" kwa Kiarabu na hutumiwa kukumbuka wakati nabii
Ibrahimu alipotaka kumtoa kafara mwanawe Ishmael alivyoamriwa na Allah, lakini
akapewa kondoo na Mungu amtoe kafara badala yake.
Sikukuu ya
Eid ul-Adha huadhimishwa kuanzia siku ya 10 tangu kuonekana kwa mwezi wa Dhul
Hijjah.






0 Maoni