Makamo wa Pili wa Rais
wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla amewataka wananchi wa Zanzibar
kuendelea kuchukua tahadhari juu maradhi ya Covid-19 yanayoendelea kuwa tishio
Duniani.
Mhe. Hemed ameleza
hayo mara baada ya kukamilika kwa ibada ya sala ya Ijumaa aliyojumuika na
waumini na wananchi wa Mwera katika Masjid Suud uliopo Regeza Mwendo wilaya ya
Magharibi “A” Unguja.
Amewakumbusha waumini
na wananchi kwa ujumla kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maradhi hayo kwa
kufuata kikamilifu maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa Afya nchini ili
kujikinga na athari zitokanazo na ugonjwa huo.
Aidha, Makamu wa Pili
wa Rais amewataka wananchi kuachana na maneno ya kasumba yanayotolewa na baadhi
ya watu mitaani ambao hawana utalamu na masuala yanayohusina na mambo ya Afya.
“Wapo watu wanatia
kasumba katika kuchukua tahadhari dhidi ya chanjo, naomba musiwasikilize”
Alieleza Makamu wa Pili wa Rais
Ameleza kuwa, suala la
kuchukua chanjo juu ya maradhi ya Covid-19 bado kwa upande wa serikali suala
hili limendelea kuwa jambo la hiyari na hakuna mtu atakaelazimishwa lakini kwa
watu wanaohitaji chanjo hiyo amewaomba kufuata taratibu zinavyoelekeza ili
waweze kupatiwa huduma hiyo.
Akigusia juu ya suala
la madawa ya kulevya Makamu wa Pili wa Rais amewataka wananchi kuendelea kutoa
ushirikiano katika kupiga vita uwingizaji, usambazaji na utumiaji wa madawa
hayo kutokana na athari mbaya zinazosababisha kupotea kwa nguvu kazi ya Taifa.
Ameleza kwamba,
serikali imejipanga kutokomeza kabisa jaanga hilo kwa kuchukua hatua kali kama
ilivyochukua hatua dhidi ya vitendo vya udhalilishaji ikiwemo kufanya
marekebisho kwa baadhi ya sheria mbali mbali.
“Jambo hili halina
msingi mzuri hapa kwetu Zanzibar” Alisema Mhe. Hemed
Pamoja na mambo
mengine Mhe. Hemed amewakumbusha wananchi kuendeleza ushirikiano na mshikamano
mingoni mwao ili kuunga mkono jitihada za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Barza la Mapinduzi DK. Hussein Mwinyi kwani kufanya hivyo kutasaidia kuchochea
kupatikana kwa maendeleo.
Nae, Khatib wa Sala ya
Ijumaa Sheikh Ahmed Khamis Bilali amewakumbusha waumini kuendelea kuhurumiana
katika masuala mbali mbali kwa kusaidiana na kutekeleza mambo mema kwa lengo la
kupata radhi kutoaka kwa Allah (S.W).




0 Maoni