Katika salam zake hizo
Mhe.Asiya amemzungumzia Marehemu Anna Mgwira kuwa alikua mwanamke Mpambanaji na
aliekuwa akijitoa katika kipindi chake chote cha uongozi alipokuwa Mkuu wa Mkoa
wa Kilimanjaro
Amesema Taifa
limepoteza Mtu Muhimu ambae alikuwa Mzalendo wa Taifa lake na Mpenda maendeleo
aliekua akisimama katika kutatua Changamoto zilizokuwa zikiwakabili wananchi
‘’kiukweli Anna Mgwira
licha ya kuwa nimemfahamu mda mrefu
lakini pia alikua mwanachama mwenzangu wa Chama cha Mapinduzi,kwahyo nasema
nimpambanaji na aliekuwa akijituma katika majukumu yake na tumeshuhudia kipindi
cha Uongozi wake Mkoa wa Kilimanjaro alikua akishuhulika sana na kutatua
changamoto za Wananchi bila kumbagua mtu kwa itikadi ya chama ama Dini’’alisema
Mhe.Asiya Sharif
Anna Elisha
Mghwira, amefariki dunia leo wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya
Mount Meru Arusha
Imeelezwa kuwa Mama Mghwira amefariki dunia leo
Julai 22, 2021, majira ya mchana, ambapo taarifa zinadai kwamba wiki moja
iliyopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua
ambapo baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru
hadi umauti ulipomkuta.





0 Maoni