Naibu Waziri wa Fedha
na Mipango, Mhandisi Hamad Masauni, ametoa angalizo kwa baadhi ya Kampuni za
simu kwa namna zinavyofanya promosheni zao kuhusu kodi ya Serikali kwa njia ya
miamala kwa kutoa taswira mbaya pekee na sio faida zitakazo mgusa mwananchi
moja kwa moja.
Akizungumza na Mabalozi Uhamasishaji wa Ulipaji Kodi kwa Hiari walioteuliwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigylu Nchemba kwa nyakati tofauti.
Mhandishi Masauni amesema, huduma ya makato ya miamala kutoka kampuni za mawasiliano imekuwa ikitozwa kwa anaetoa na anaepokea hivyo sio jambo geni.
Ameongeza kuwa tayari Rais Samia alishatoa maelekezo kwa Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu kuunda timu ya wataalamu ili waweze kuona namna bora ya kuboresha kodi hiyo ikiwa ni pamoja na kuangalia marekebisho ya sheria.





0 Maoni