Katibu Mkuu Wizara Afya,Ustawi wa Jamii Wazee,wanawake na watoto Dkt.Omar Dadi Shajak(kushoto)

Jopo la Madaktari bingwa wa wanaotarajiwa kutoa  huduma za  matibabu ya upasuaji na maradhi mengine, kutoka nchini Saudia Rabia wamewasili Kisiwani Zanzibar kwa ajili ya utoaji wa huduma hiyo kwa Wananchi wanaoishi Kisiwani kuanzia Terehe 24-07-2021 .  

Akitoa taarifa kwa wandishi wahabari mbele ya madaktari hao waliowasili ofisini kwake Mnazi Mmoja, kwa niaba ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee,Jinsia  na Watoto,  Katibu  Mkuu Wizara hiyo, Dkt.Omar Dadi Shajak amesema, madaktari hao watakua kisiwani Pemba kwa muda wa siku tano kwaajili ya Utoaji huduma za Upasuaji na Maradhi ikiwemo Henia na Maradhi mengine

Katika hatua nyengine Katibu Omari amewataka wananchi Kisiwani Pemba Kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kupata hudma kutoka kwa madaktari hao ambao wamebobea katika masuala la Upasuaji ili waitumie vyema  fursa hiyo kwa maslahi ya afya zao.

 Nae kiongozi wa msafara wa madaktari hao Dkt.Yussuf Al alawi alimueleza Dkt Shajak kwamba, wamekuja kutoa huduma hiyo muhimu kwa wananchi na wataanzia katika kisiwa cha Pemba.

 Aidha alisema wataisadia hospitali ya Wete kwa kuipatia vifaa vya upasuaji wa maradhi ya mifupa ili kuondoa usumbufu wa kufata huduma izo Unguja.