uboresha kilimo cha biashara chenye tija.
Aidha kuboreshwa kwa kilimo hicho kutasaidia
kuwapo kwa usalama wa chakula na kuongeza pato la kaya.
Hayo yameelezwa mwishoni mwa wiki baada ya
ujumbe wa AGRA ukiongozwa na Waziri Mkuu Mstaafu wa Ethiopia na
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa AGRA, Hailemariam Dessalegn, kumtembele
Rais Mstaafu katika taasisi yake ( Jakaya Mrisho Kikwete Foundation -JMKF)
iliyopo mkoani Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete
alitaka kusaidiwa kwa wajasiriamali ambao ni muhimu katika kufanikisha viwanda
vya mnyororo wa kilimo nchini.
"Ili kuwepo na mabadiliko ya kilimo ni
muhimu kwa viwanda vidogo kufahamu soko lao vyema na wao kuwekwa mstari wa
mbele katika kubadili kilimo," alisema Kikwete, ambaye pia ni mjumbe wa
bodi ya AGRA chini ya uenyekiti wa Dessalegn.
Mkutano huo wa mwishoni mwa wiki pia
ulihudhuriwa na Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Faustine Mkenda, Waziri wa
Biashara na Viwanda Profesa Kitila Mkumbo.
Profesa Mkumbo katika mazungumzo
hayo alielezea vipaumbele vya wizara yake katika kuongeza tija kwenye kilimo na
kushukuru AGRA kwa kushawishi kuondolewa kwa Kodi ya Thamani (VAT) kwa baadhi
ya zana za utunzaji wa mazao baada ya mavuno.
Dessalegn na ujumbe wake uliwasili nchini
Ijumaa kwa ziara ya siku tano ambapo anatarajiw akukutana na Rais Samia
Suluhu Hassan kwa mazungumzo kuhusu mfumo wa chakula.
Mazungumzo hayo ni muhimu wakati bara la
Afrika linajiandaa kuwasilisha taarifa yake katika mkutano wa mifumo ya chakula
wa Umoja wa Mataifa baadaye mwaka huu.





0 Maoni