Uongozi wa klabu ya Yanga Sc umethibitisha kuwa
tayari wamewasilisha ushahidi wa kesi dhidi ya mchezaji Bernard Morrison na
kinachosubiriwa sasa ni kutolewa hukumu kwa kesi hiyo
Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa Michezo (CAS)
inatarajiwa kutoa hukumu ya kesi hiyo kabla ya mwezi huu kumalizika
Uamuzi wa Kesi hiyo Inaelezwa itatolewa maamuzi na
CAS Julai 22 na Jaji kutoka nchini Uingereza
Mapema wiki hii katika mahojiano katika kituo kimoja
cha Tv Jijini Dar Es Salam, Afisa Habari wa Yanga Sc Hassan Bumbuli alizungumza
kuwa Yanga Sc itakuwa bingwa msimu huu na jambo hilo litatokea kabla ya Julai
25 siku ya mchezo wa fainali kombe la FA
"Tuna michezo miwili kukamilisha msimu, Julai
14 tutacheza na Ihefu Fc na Julai 18 Dodoma Jiji, tunahitaji kushinda mechi
zote mbili. Naamini tutakuwa mabingwa msimu huu, tena jambo hilo litatimia
kabla ya mchezo wa fainali ya FA," alitamba Bumbuli





0 Maoni