Mkuu wa wilaya ya
magaharib A Suzan Peter Kunambi ameutaka uongozi wa shule ya
mbuzini na kamati ya skuli hiyo kuondosha tofauti zao ambazo zinazopelekea
migogoro ya chini kwa chini ili kuepusha kurudisha nyuma maendeleo
ya elimu katika skuli hiyo.
Akitoa kauli hiyo wakati akisikiliza changamoto za skuli katika kikao cha pamoja kati ya wazazi kamati ya skuli na walimu kilichofanyika skuli ya mbuzini.
Amesema kuendelea kwa mgogoro hiyo hasa wakati huu ambapo wanafunzi wanajiandaa na mitihani ya Moko na Mitihani ya Taifa si jambo jema kwani kutazorotesha maendeleo ya skuli hiyo na kupunguza kiwango cha upasishaji kwa wanafunzi.
Nao wazazi waliohudhuria Kikao hicho wamesema watalitekeleza kwa vitendo agizo la Mkuu wa Wilaya kuondosha Migogoro katika Shule hiyo ili kuongeza ufaulu kwa watoto wao.





0 Maoni