Zanzibar
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo amesikitishwa na uwepo wa idadi kubwa ya
bodaboda katika Vituo mbalimbali vya Polisi nchini huku akiwaasa wananchi ambao
mashauri yao yanasikilizika wafike katika vituo hivyo ili kuondoa msongamano wa
vyombo hivyo.
Ameyasema hayo leo
Visiwani Zanzibar baada ya kupata maelezo na kutembelea karakana ya kuhifadhia
vidhibiti hivyo katika Kituo cha Polisi Madema ambapo amesikitishwa na wingi wa
bodaboda kituoni hapo.
“Nchi yetu inataka
kupiga hatua za kmaendeleo na uchumi, kwa namna hii ya mrundikano wa bodaboda
katika vituo vya polisi maana yake shughuli nyingi huko za vijana zimesimama,
naelewa kuna vidhibiti kwa ajili ya kesi maalumu ambazo nyingine ziko mahakamani
hivyo haviwezi kuachiwa lakini kwa vile ambavyo kanuni na sheria inaweza
kuviruhusu basi viondoke, natoa wito kwa wananchi kufika vituo vyote vya polisi
nchi nzima na kufanya mazungumzo na wakuu wa vituo ili tuondoe mrundikano
huu,kila mkoa ninaotembelea nakuta vituoni kuna mrundikano wa bodaboda,wananchi
njooni muonane na wakuu wa vituo mchukue vyombo vyenu”alisemam Naibu Waziri
Chilo
Akizunguma katika
ziara hiyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Unguja, Awadh Juma Haji amesema
vyombo vingi vilivyopo kituoni ni kutokana na waliovitendea makosa kutofika
vituoni kwa wahusika wakuu hali inayopelekea uwepo wake hapo ambapo alikiri
imekua ni kero kwa jeshi la polisi.
“Mheshimiwa Naibu
Waziri hapa vyombo vilivyopo ambavyo tunavishikilia hatuwezi kuvitoa ni vile
ambavyo mashauri yake bado yapo mahakamani lakini kuna vingine watuhumiwa wake
wamekimbia tangu vikamatwe bado awajajitokeza tunachofanya tunasubiri ule muda
wa kisheria wa miezi sita ili taratibu za utaifishaji zifanyike hapa tuna
magari ya wizi,bodaboda nyingine zimeshiriki katika makosa ya usalama
barabarani nyingine zimehusika kwenye uporaji na tatizo linguine wahusika
hawaji vituoni kuonana na wakuu wa vituo kuchukua vyombo vyao hali hiyo
upelekea mrundikano huu.”alisema RPC Awadh
Akitoa hali ya ulinzi
na usalama katika Kipindi hiki cha Sikukuu Kamanda Awadh amesema Sikukuu ya Eid
imesheherekewa vizuri pasipo kuwepo matukio makubwa ya uhalifu huku Jeshi la
Polisi likiendelea na doria zake za kawaida katika kuhakikisha amani na usalama
vinakuwepo katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar.




0 Maoni