Hayo yameelezwa hapo Jana na Makamo wa Pili wa Raisi wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibara Mh Hemed Suleiman Abdullah katika Viwanja vya
Konde Mjini ,Mkoa wa Kasakazi Pemba, wakati akifunga kampeni za kumnadi mgombea
nafasi ya ubunge wa Chama cha mapinduzi .
Amesema tayari
Serikali imejianda karibuni kuwaleta wakandarasi katika maeneo yote ya Barabara
yaliyoainishwa Unguja na Pemba kwaajili ya kuanza ujenzi ambapo Kilometa Zaidi
ya Mia nne na Ishirini zikiwemo Barabara Kuu na zile za Ndani zinataraajiwa
kujengwa kwa kiwango cha Lami.
Amezitaja baadhi
ya barabara zitakazonufaika kwa upande Jimbo la Konde ni Konde- Msuka,Konde Makangale,Konde-Kipange
na Konde- Ungi ,ambapo amesema ujenzi huo utaanza na kukamilika kwa muda mfupi
kutokana na barabara nyingi kilometa zake kutokuwa na ubali mrefu.
Katika hatua
nyengine Mh Hemed amewataka wananchi wa
Jimbo la Konde kumchagua Mgombea wa nafasi ya Ubunge atokanae na Chama cha
Mapinduzi (CCM) ndugu Sheha Mpemba Faki ili akasimamie yale ambayo Serikali ya
Ccm imedhamiria kuyafanya katika Jimbo hilo
Amesema kufanya
hivyo wataweza kulifanya Jimbo la Konde kupiga hatua za kimaendeleo kwakua
Mgombea huyo atokanae na Chama cha Mapinduzi nimchapa kazi na anajua shida za
wananchi wa Konde.
Uchaguzi Mdogo kuziba nafasi ya Ubunge katika Jimbo la
Konde unatarajiwa kufanyika kesho tarehe 18-07-2020 ambapo uchaguzi huo unfanyika
kufuatia kufariki Dunia kwa aliyekua Mbunge wa Jimbo hilo Mh Khatib Said Haji
Alhamis ya Mei 20.
wabunge na wawakilishi wa Kisiwan Pemba watokanao na Chama cha Mapinduzi wakifurahia jambo katika shuhuli za kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Konde Mh Sheha Mpemba Faki




0 Maoni