Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kufanya mazungumzo na
Naibu Waziri Mambo ya Nje wa Poland anayeshughulikia na masuala ya Siasa,
Uchumi na Maendeleo kwa nchi za Afrika Mhe.Pawel Jablonski ofisini kwake jijini
Dodoma.
Akiongelea kikao hicho Balozi Mbarouk amesema kuwa
wamejadiliana juu ya kuimarisha mahusiano yaaliyopo kati ya Tanzania na Poland
ikiwa ni pamoja na kuanzisha uwekezaji mpya nchini, kuwezesha wanafunzi na
wataalamu wetuu kujifunza na kupata utaalmu hasa katika matibabu ya moyo,
masikio, pua na Koo.
“Tumekutana hapa na Mhe naibu Waziri kutoka nchini
Poland, tumezungumza na kujadiliana juu ya namna bora za kuendelea kuimarisha
mahusiano baina ya nchi zetu , tuna maeneo mengi ambayo tunashirikiana baina ya
nchi zetu, lakini pia nimewaomba kuanzisha uwekezaji mpya nchini, ikiwa ni
pamoja na kutoa nafasi za masomo kwa ameneo ya matibabu ya moyo, masikio,pua na
koo”, amesema Balozi Mbarouk.
Amesema kuwa wamejadiliana juu ya kuhakikisha ujenzi
wa Kiwanda cha matrekta cha Kibaha na ujenzi wa maghala ya kuhifadhia nafaka na
kuongeza kuwa ujio wa Naibu Waziri huyo utawezesha kukwamua miradi hiyo na
hivyo kuikamilisha kama ilivyopangwa
Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri huyo
ameelezea utayari wa Poland katika kuhakikisha mahusiano kati ya Poland
na Tanzania yanaimarika na kuendelea kuisaidia Tanzania katika sekta za
elimu, kilimo hasa ikizingatiwa kuwa Poland imeendelea kwa kiasi kikubwa
kupitia kilimo.
Amesema Poland iko tayari kuisaidia Tanzania kaatika
maeneo ya elimu kwa kutoa nafasi za masomo nchin Poland ikiwa ni pamoja na
ufadhili kwa wanafunzii wa Kitanzania, uwepo wa mifumo ya kisasa ya
kutolea maji taka, kilimo na maendeleo ya usalama wa chakula.
Naibu Waziri huyo. Mhe. Powel yuko nchini kwa
ziara ya kikazi ya siku nne ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani
Dkt. Abdallah Possi pamoja na Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka nchni Poland
waliobobea katika maeneo ya teknolojia ya kisasa katika sekta za kibenki (smart
teknologies) teknolojia ya kisasa katika sekta ya umeme (smart technologies for
electricity sector -smart meter connection and lighting systems) na ulipaji kwa
kutumia teknolojia za kisasa (smart payment apps).
Naibu Waziri huyo na timu wanatarajia kutembelea Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shirika la Umeme nchii (TANESCO)
Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Benki za CRDB na NMB na Shirika la
Hifadhi za Jamii (NSSF).
Ziara ya naaibu Waziri huyo imefuatia mwaliko
uliotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia
Idara ya Ulaya na Marekani







0 Maoni